Skip to content

Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine

KSh 487.20

Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi wa kipekee kwani umewashirikisha waandishi wenye tajriba pevu katika fani ya uandishi na kuwapa nafasi waandishi wachanga katika tasnia ya uandishi wa kifasihi. Waandishi waliochangia katika mkusanyiko huu wameonyesha ubunifu mkubwa kwa kusawiri uhalisia wa maisha katika mazingira yao tofauti tofauti. Suala la uhalisia wa maisha na mwingiliano wake na fasihi haliwezi kupuuzwa kwani fasihi ni kioo cha jamii.

Mkusanyiko huu una hadithi zenye maudhui mbalimbali na zinazosheheni migogoro itakayowafikirisha wasomaji. Hali kadhalika, huu ni mkusanyiko wa kwanza wa hadithi fupi kuwahi kuchapishwa ulio na idadi karibu sawa ya waandishi wa kike na wa kiume.

D. W. Lutomia na Phibbian Muthama, ambao ndio wahariri wa mkusanyiko huu ni watunzi wa kazi bunilizi za fasihi wenye tajriba pana. Wana mchango mkubwa katika ufundishaji wa fasihi na sanaa nyinginezo.

Long Description

Product Details

Related Products